Mo Aomba Uwanja wa Taifa Upewe Jina la Mkapa

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba SC, Mo Dewji leo ameomba watu kumuunga mkono kumshawishi Raisi John Magufuli kuwa Uwanja wa Taifa kuitwa Benjamin William Mkapa kama sehemu ya kumbukumbu ya mchango wake katika ujenzi wa uwanja huo. ”Leo nimeamua kuanzisha petition (maombi) kwa Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Magufuli kubadili jina la Uwanja wa Taifa kuwa: Uwanja wa Benjamin William Mkapa.

Ujenzi wa Uwanja wa Taifa wa jijini Dar es Salaam ulianzishwa na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin William Mkapa. Uwanja huo wenye uwezo wa kubeba mashabiki 60,000 ni miongoni mwa viwanja bora katika bara la Afrika kwa sasa. Uwanja huo kwa namna mmoja au nyingine umesaidia kuendeleza mpira wa miguu na michezo mingine nchini Tanzania. Uzuri na ukubwa wa soka letu umedhihirishwa kwa sababu ya uwanja wetu huo ambao unashika nafasi ya 11 kwa ukubwa Afrika.


Uwanja huo wa kisasa umeongeza uzalendo mkubwa kwa kuwezesha maelfu ya mashabiki kuwa sehemu ya michezo yote mikubwa, pia umeongezea mapato kwa klabu zote na kutuletea heshima kubwa nchini na mifano ipo dhahiri. Kutokana na uzuri wa uwanja huo, klabu zote za nje ambao huja kucheza katika uwanja huo zimekuwa zikitoa sifa mbalimbali. Timu za mataifa makubwa kama Brazil zimecheza kwenye uwanja huo na kumwaga sifa mbalimbali.

Nje ya michezo, mashindano ya usomaji wa Quran yaliona mkusanyiko mkubwa zaidi kwenye mashindano makubwa ya kusoma Quran barani Afrika, hii nayo ilikuwa ni rekodi nzuri kwetu Watanzania. Nje ya michezo, mashindano ya usomaji wa Quran yaliona mkusanyiko mkubwa zaidi kwenye mashindano makubwa ya kusoma Quran barani Afrika, hii nayo ilikuwa ni rekodi nzuri kwetu Watanzania.

Tumeshuhudia matamasha mbalimbali makubwa kama matamasha ya Pasaka na Krsimasi yakifanyika hapo na lengo la yote hayo ni kuleta umoja na mshikamano miongoni mwa Watanzania. Itakuwa ni heshima kubwa kama uwanja wetu pendwa utaitwa jina la Uwanja wa Benjamin William Mkapa. Tunamuomba Rais John Pombe Magufuli aridhie kubadili jina la uwanja huo kwa heshima ya Hayati Mkapa ili tuendelee kumkumbuka kwa mchango wake mkubwa na hasa kwa vizazi vijavyo.

Tunawaomba Watanzania wote bila kujali ushabiki wa klabu muunge mkono kwa kuweka sahihi ili tumuombe Mhe Rais kubadilisha jina la uwanja huo uitwe Benjamin William Mkapa Stadium au Uwanja wa Benjamin William Mkapa.”


Nini kinachokupa raha kama michezo ya kasino ya mtandaoni? Hasa unapojua kuwa kuna ushindi, jackpot na mizunguko kibao ya bure.
Ungana na bwana Meridian kupata ushindi na burudani.

Cheza Hapa Sasa

43 Komentara

    Ni wazo zuri sana #Meridianbettz

    Jibu

    Mawazo yake nimeyaelewa

    Jibu

    Kwa alilolisema dewji ni la kweli ingependeza jina la mkapa kuwepo Ili kumuenzi

    Jibu

    Sio mabaya mawazo yake

    Jibu

    wazo zuri hii itasaidia vizazi vijavyo kwaajili ya kumbukumbu

    Jibu

    wazo lake ni zuri

    Jibu

    Inabidii hilo wazo litendewe kazi kwa kweli

    Jibu

    Tajiri kashasema

    Jibu

    Wazo lake Ni sahihi

    Jibu

    Mawazo yake Mo nimeyakubali yapo sahii akika naili wanaweza wakalipitisha kwangazi zajuu

    Jibu

    Ni sawa wazo lako mo ili tuendelee kumuenzi

    Jibu

    Ni wazo zuri na lenye mashiko katika Taifa letu, Binafsi namuunga mkono yani kwa Mzee Mkapa itapendeza sana.

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Wazo lake ni sahihi

    Jibu

    Mawazo mazuri ila uwamuzi tuwaachie serikali

    Jibu

    Hajakosea kuomba ivo ila amecherewa sana tushazoea kuita uwanja wa taifa

    Jibu

    Itakua kumbukumbu nzuri

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Wazo zuri

    Jibu

    Sawa tu,likiwekwa jina la mkapa.

    Jibu

    sio mbaya

    Jibu

    Mawazo yake tu sio lazma yatimie

    Jibu

    Wazo zuriiii

    Jibu

    Siyo mbaya

    Jibu

    Lilikuwa wazo la Mkapa Uwanja wa kisasa ujengwe jambo ambalo tulidhani haliwezekani kwa miaka mingi. Ni jambo la heshima uwanja kupewa jina la hayati Mkapa kumuenzi#meridianbettz

    Jibu

    Ni vizur kufanya ivyo inaleta heshimaa!!

    Jibu

    Kwl wawez kumuwenz mzee wetu na kumpa heshimah yake

    Jibu

    Itakua kumbukumb nzur zaid

    Jibu

    Sio jambo baya .

    Jibu

    Kwani kabla ya apo sindio unavyoitwa uwanja wa mkapa na sio wa mchina

    Jibu

    Tajiri mo tupo pamoja na wewe kwa wazo lako#meridianbettz

    Jibu

    Ni jambo zuri

    Jibu

    Mawazo yake yafanyiwe kazi

    Jibu

    Yuko sahihi kwa mawazo yake

    Jibu

    kila na mtu na mawazo yake

    Jibu

    Sio mbaya lakini#Meridianbettz

    Jibu

    Litakua jambo bora sana kwani kumbu kumbu zake zitakua kwa vizazi vijazo na mchango wake katika nyanza za michezo.

    Jibu

    Sio mbaya

    Jibu

    Moo yupo sahihi itakuwa km kumbu kumbu za kumuenzi mh mkapa

    Jibu

    Mo yupo sahih

    Jibu

    Aliomba hivyo na umekuwa hivyo so toka Sasa ni mkapa stadium

    Jibu

    Mawazo take yamekubarika

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.