Kiungo mshambuliaji wa Yanga,Feisal Salum amesema kuwa baada ya kumaliza ahadi ya kwanza kwa wanayanga kwa kuhakikisha kuwa wanabeba makombe msimu huu, ahadi iliyobaki kwao ni kuhakikisha kuwa wanafanya vyema katika michuano ya kimataifa kwa msimu ujao.

Yanga katika michuano ya kimataifa kwa msimu uliopita walitolewa katika hatua ya awali dhidi ya Rvers ya nchini Nigeria.

Feisal alisema kuwa baada ya kukamilisha ahadi yao kwa mashabiki wa itimu kwa kuhakikisha kuwa wanatwaa mataji sasa kilichobaki kwao ni kuhakikisha kuwa wanafanya vizuri katika michuano ya kimataifa na kufika katika hatua ya mbali na msimu uliopita.

“Lengo la kwanza tumelikamilisha ambalo lilikuwa ni kuihakikisha kuwa tunafanya vyema kwa kutwaa mataji kama ya ligi kuu na kombe la Shirikisho yaani FA,tunashukuru kwa kuwa tumeweza kukamilisha ahdai hiyo ambayo ilikuwa inatuumiza kichwa lakini tulipambana kisha tukaifanikisha.”

“Kwa sasa tuna deni kubwa kwa wanayanga kwa kuhakikisha kuwa tunafanya vyema katika michuano ya kimataifa ambapo msim,u ulioopita hatukuweza kukamilisha ahadi hiyo kwa kuwa tuliweza kutolewa katika hatua yua mapema zaidi,msimu ujao tutahakikisha kuwa tunafika mbali,tutafanya kila namna tufike mbali zaidi,”alisema kiungo huyo.”


 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa