UONGOZI wa Pan African unatarajia kufanya kikao cha viongozi na wanachama wa klabu hiyo kwa ajili ya kuweka mikakati ya msimu ujao. 
Pan ambayo inadhaminiwa na kampuni ya Meridianbet itashiriki michuano ya Championship kwa msimu ujao wa 2022/23.
Katibu wa Pan, Abbas Ally amesema kuwa
“Tutakuwa na kikao kesho, Alhamis kitakachohusisha wanachama na wadau wa Pan African kuanzia saa 4:00 asubuhi kwenye ukumbi wa Falcon Hotel, Lumumba, Dar.”
“Lengo la mkutano huo ni kujadili masuala mbalimbali yaliyojitokeza kwa msimu uliopita na kupanga mikakati ya msimu ujao pamoja na namna ya kuboresha kikosi chetu.”
Msimu uliopita ulikuwa una changamoto kwa klabu hii, bila shaka watajipanga vyema kurejea kwenye michuano ya Championship kwa msimu mpya.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa