BAADA ya kuhusishwa na uhamisho wa Simba, beki wa Biashara United ya Mara, Abdulmajid Mangalo amefunguka kukataa ofa hiyo huku akitarajia kujiunga na klabu nyingine.
Licha ya Biashara United kushuka daraja lakini beki huyo alionyesha kiwango bora kiasi cha kuzishawishi baadhi ya klabu za ligi kuu kuhitaji huduma yake kwa msimu ujao.
“Kwa sasa nipo mkoani Mara ambao naendelea na majukumu yangu mengine ila mkataba wangu na Biashara ulimalizika mwishoni mwa msimu huu.”
“Siwezi kuendelea kubaki ndani ya Biashara kwani zipo klabu nne za ligi kuu ambazo zimenipa ofa ila siwezi kujiunga na timu za kariakoo lakini nitaenda timu nyingine.”