Klabu ya Biashara United inayoshiriki ligi kuu ya NBC Premier League imefungiwa kufanya usajiri kwa muda wa miaka miawili baada ya kukaidi maamuzi ya shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA la kumlipa stahiki zake mchezaji wake Timoth Balton Omwenga.

Timoth Balton Omwenga alipeleka shauri lake FIFA, baada ya klabu ya Biashara United kushindwa kumlipa stahiki zake ambazo alipaswa kualipwa baada ya kuitumikia klabu hiyo,  baada ya kushinda shauri lake, FIFA iliamuru alipwe stahiki zake ambazo mpaka sasa klabu hiyo haijalipa.

Biashara United

Waraka uliotumwa na FIFA kwenye shirikisho la soka nchini TFF, imeamauru klabu ya Biashara ifungiwe kusajiri kwa takribani misimu miwili, kwa kukaidi maamuzi ya shirikisho hilo la mpira wa miguu duniani.

Uamuzi wa awali ambao FIFA waliutoa kwa klabu ya Biashara United, ni kuwazuia kutokufanya usajiri wowote mpaka pale watakapokamilisha malipo ya Timoth Balton Omwenga.

Klabu ya Biashara United kwenye msimamo wa ligi kuu ya NBC inashika nafasi 15, ambapo iko kwenye hatari ya kushuka daraja msimu huu.


ALIYA’S WISHES

Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa