Inaelezwa kuwa Kocha Mkuu wa Azam FC inayotumia Uwanja wa Azam Complex kwenye mechi za nyumbani Rachid Toussi atakutana na Thank You baada ya msimu wa 2024/25 kugota mwisho na mabosi wa timu hiyo wameshafanya maamuzi.

Taarifa zinaeleza kuwa Azam FC wanasubiri msimu uishe kwa mechi mbili ambazo zimesalia kukamilisha msimu ambapo watakuwa na mchezo mmoja wa funga kazi wakiwa Azam Complex na itakuwa dhidi ya Tabora United, Juni 18 2025 na ule wa mwisho ni dhidi ya Fountain Gate, Juni 22.
Mbali na kocha Toussi, wasaidizi wake Badr Driss, kocha wa viungo Ouajou Driss na kocha wa makipa Rachid El Mekkaoui nao watapewa Thank You, hivyo matajiri hao wataanza msimu na benchi jipya la ufundi. Ikumbukwe kwamba kocha wa Azam FC alipewa mkataba wa mwaka mmoja akichukua mikoba ya Yusuph Dabo.
Bila kusahauΒ meridianbetΒ ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa

Azam FC kwa msimu wa 2024/25 imepishana na mataji yote iliyokuwa ikipambania kuanzia lile la Ligi ya Mabingwa Afrika, Ligi Kuu Bara, CRDB Federation Cup kwa kuwa ilipofungashiwa virago na Mbeya City.
Hasheem Ibwe, Ofisa Habari wa Azam FC alibainisha kuwa wamepoteza kila kitu ambacho walikuwa wanapambania hivyo watajipanga kwa ajili ya msimu mpya kufanya vizuri


