Klabu ya Barcelona imetanganza kukamilika kwa usajili wa kiungo wa Ivory Coast, Franck Kessie na beki wa Denmark Andreas Christensen kwa uhamisho wa bure.

Christensen amejiunga na Barca akitokea Chelsea ambako mkataba wake umemalizika mwishoni mwa msimu uliyoisha baada ya kuitumikia klabu hiyo ya London kwa takribani miaka 10 akifanikiwa kucheza mechi 161 na kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa, Europa, na mataji mengine ya ndani.

Wakati kwa upande wa Kessie amejiunga na The Blaugrana akitokea AC Milan ambao alijiunga nao tangu mwaka 2015 na alifanikiwa kufunga mabao 7 kwenye michezo 39 msimu uliyopita ambapo Milan walitwaa Scudetto kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2011.

Wachezaji wote watatambulishwa kwa mashabikindani ya wiki hii ambapo Kessie atatambulishwa Jumatano na Christensen itakuwa Alhamisi.


BASHIRI HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa