Kiungo nyota wa klabu ya Manchester City Bernardo Silva ameweka wazi nia yake ya kutaka kujiunga na klabu ya Barcelona msimu huu na tayari ameshafanya mazungumzo na wakala wake kuhusu swala hilo.

Klabu ya Barcelona imekuwa ikimfuatilia kwa muda mrefu mchezaji wa kimataifa kutoka nchini Ureno silva, na kwa sasa ananaoneka kuwa ndio mbadala sahihi ikiwa watamapomteza kiungo wao Frenkie de Jong, ambaye muda wowote kuanzia sasa anaweza kujiunga na Manchester United.

Bernardo Silva

Ijapokuwa, kwa sasa Bernardo Silva bado ana mkataba na klabu ya Manchester City ambao unatarajiwa kuisha mwaka 2025, lakini Pep Guardiola hana mpango wa kumuweka sokoni kwa sasa.

Bernardo Silva msimu huu ameichezea klabu ya Manchester City michezo 50 kwenye mashindano yote, huku akifanikiwa kufunga magoli 13. Pia Silva ametajwa kwenye kikosi cha ‘PFA Premier League Team of the Year’.


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa