Mpango huu pia umepangwa kuanzishwa kwenye michuano ya wanawake ya Women’s Championship kuanzia Julai 6.
kwa mujibu wa UEFA, kampeni hii itaenda sambamba na kampeni ya “Real Scars” ikiwa inalenga kuielimisha jamii juu ya athari za unyanyasaji wa mtandaoni dhidi ya wachezaji, makocha na maafisa wengine kupitia mitandao ya kijamii.
Jorginho amenukuliwa akisema
“Unyanyasaji wa mtandaoni ni mbaya sana kwa sababu watu hawafikirii juu ya athari wanazosababisha. Unaweza kukuathiri wewe pamoja na watu wanaokupenda.”
Ripoti moja kutoka chapisho la Italia ilitaja kuwa Paulo Dybala, ambaye kwa sasa ni mchezaji huru baada ya kuachana na juventus na kuhusishwa zaidi na Inter, ameamua kuzima taarifa za instagram kwa sababu ya jumbe alizokuwa anapokea.
UEFA pia wanatoa Makala inayoelezea athari za unyanyasaji wa mtandaoni, ambayo itawahusisha aliyewahi kuwa kiungo wa Juventus na Inter Patrick Vieira pamoja na Jesús Tomillero Benavente, refarii wa Hispania aliyeamua kustaafu kwa ajili ya unyanyasaji wa mtandaoni