Taarifa zinasema kuwa ni matamanio ya Joan Laporta kuona nyota Frenkie de Jong anasalia Barcelona, lakini bado kuna changamoto mahali.

Laporta anajaribu kujanusha kuwa yeye hapendi kuona klabu yake imeshindwa kumbakiza staa huyu, Hata hivyo,inaonekana kuwa suala la mishahara klabuni hapo bado linaendelea kuwatatiza Barcelona.

Katika hali ambayo Barceola wapo sasa hivi, ofa ya Man United kumsajili Frenkie de Jong inaonekana kuwa ofa bomba kabisa kwa Barca.

Laporta amenukuliwa akisema:

“Nitafanya kila niwezalo kumbakiza Frenkie, lakini pia ni suala la mshahara, na hilo lazima lirekebishwe. Ni mchezaji wa Barca, mmoja wa wachezaji bora zaidi duniani kwa nafasi yake sasa.”

“Tunajua kuna vilabu vinamtaka, sio United pekee, lakini hatuna nia ya kumuuza. Anataka kubaki, yuko vizuri Barcelona, na nitafanya kila niwezalo kumfanya abaki.”


JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa