Klabu ya Bayern Munich wanaonekana kama wamepunguza nia yao ya kutaka kumnasa mshambuliaji wa Liverpool Sadio Mane baada ya mkurugenzi wa michezo wa klabu hiyo Hasan Salihamidzic kusema kwamba Mane sio uchaguzi pekee ambao Bayern Munich wanategemea.
Mane aliijulisha Liverpool kwamba anataka kuihama klabu hiyo wakati wa dirisha hili la majira ya kiangazi na Bayern walionekana kuvutiwa na Msenegali kuwa kama mbadala wa Lewandowski ambaye pia aliifahamisha Bayern kwamba anataka changamoto mpya.
Lakini upande wa miamba wa Bavaria wanaangalia chaguo zaidi kuliko winga wa Senegal Mane, kama Salihamidzic aliambia BILD: “Soko la uhamisho sio rahisi na mara zote inategemea uwezo wa kifedha wa klabu.
“Kimsingi tunajaribu kuimarisha timu yetu pia tunafanyia kazi baadhi ya chaguzi kwenye safu ya ushambuliaji.
“Kwa kweli huwezi kujipunguza kwa chaguo moja, lazima uwe na chaguzi kadhaa.”
Ikumbukwe Liverpool waliikataa ofa iliyoboreshwa ya pauni milioni 23.5 ambayo inaweza kupanda hadi pauni milioni 30 kutoka kwa Bayern Munich kwa ajili ya Sadio Mane.
ALIYA’S WISHES
Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa.