Big sunday inakwenda na big match ni Manchester City vs Liverpool huku kikosi cha Pep Guardiola kikiingia kwenye mchezo huo akiwa anaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa alama 73 alama moja zaidi ya majogoo.
Tokea Guardiola achukue hatamu ya kukinoa kikosi cha Man City amefanikiwa kuchukua ubingwa wa Uingereza karibia kila msimu isipokuwa mwaka 2020, ambapo Klopp alifanikiwa kuingoza Liverpool kuchukua ubingwa wa ligi hiyo baada ya miaka 30.

Manchester city kwenye michezo 30 waliyocheza ameshinda michezo 23, sare 4 na amepoteza michezo 3 huku akifanikiwa kufunga magoli 70 huku akiruhusu magoli 18, wakati Liverpool kwenye michezo 30 ameshinda 22, sare 6 na amepoteza michezo 2 huku akifanikiwa kufunga magoli 77 na kuruhusu magoli 20 mawili zaidi ya City.
Man city na Liverpool wamekutana mara 49 kwenye ligu kuu ya Uingereza, huku Liverpool akishinda mara 20 na Man city 11 na wakitoka sare michezo 18.
Matokeo ya michezo mitano ya mwisho
- Liverpool 2-2 Manchester City (October 3, 2021)
- Liverpool 1- 4 Manchester City (February 7, 2021)
- Manchester City 1-1 Liverpool (November 8, 2020)
- Manchester City 4-0 Liverpool (July 2, 2020)
- Liverpool 3-1 Manchester City (November 10, 2019)
Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.


