Klabu ya Chelsea imemsajili beki wa Kihispania Marc Cucurella kutoka klabu ya Brighton & Hove Albion kwa kitita cha pauni milkioni 60 dili itakayo dumu kwa miaka sita.

Cucurella Asaini na Chelsea Dili ya Miaka 6

Manchester City pia walikuwa wakiiwinda saini ya mchezaji huyo wa kimataifa wa Hispania lakini The Blues  wamefanikiwa kuwazidi kete matajiri wa jiji la Manchester.

Tajiri mpya wa Chelsea Todd Boehly amefurahishwa na uhamisho huo huku akiwa na matarajio mazuri kutoka kwa mlinzi huyo wa kulia.

“Marc ni beki bora ambaye amedhihirisha ubora wake ndani ya Premier League na sasa atakuwa sehemu ya maboresho kwwenye kikosi chetu,” alisema Boehly

Cucurella pia alifurahi kukamilika kwa dili hiyo alisema: “Nina furaha sana ni fursa kubwa kwangu kujiunga na Chelsea moja ya vilabu bora ulimwenguni nitafanya kazi kwa bidii na kuisadia timu.”


EPL IMEREJEA ANZA KUWEKA MIKEKA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa