Mchezaji nyota wa Ligi ya Uingereza jina lake limehifadhiwa, alibainika kukutwa na maumivu makali kutokana na kufanya ‘ngono ngumu’ na mpenzi wake, daktari wa upasuaji kutoka Londoni Uingereza amefichua.
Nyota huyo alipelekwa kwa Profesa Aali Sheen, 51, kutoka London Kusini na daktari wa klabu yake, Ili afanyiwe upasuaji.
Mwanasoka huyo hakutaka kumwambia meneja wake kilichotokea, ambapo Mzee huyo mwenye umri wa miaka 51 alisema alikuwa bora tena baada ya wiki nne.

Akizungumza na The Sun Jumapili alisema: “Alikuwa na maumivu makali kwenye paja lake na aliniambia amekuwa akifanya mapenzi magumu na ya kutatanisha na mpenzi wake.
“Alikuwa mkweli juu ya kile kilichotokea na hata akanionyesha hali ambayo aliteseka nayo, ambayo haikuwa ya kawaida lakini yenye msaada.”Profesa Sheen alisema kuwa majeraha ya kinena huja kutokana na kujipinda na kugeuka. Pia aliongeza kuwa wakati mwingine inaweza kutokea katika hali isiyo ya kawaida.
Daktari huyo wa upasuaji, ambaye ana kitabu kinachoitwa The Painted Surgeon ambamo anataja hadithi nyingine, pia alifichua jeraha jingine la kushangaza alilokabiliana nalo.
Jeraha hilo lilimhusu mwanasoka mwingine ambaye alihitaji kufanyiwa upasuaji baada ya kuumia kwa kukohoa na kupiga chafya.
Daktari huyo mwenye umri wa miaka 51, anayejulikana kwa jina la Herniator kwa sababu ya ujuzi wake, amesaidia wachezaji takribani 3,000 wa michezo mbalimbali.
Wateja wake maarufu mara nyingi hujumuisha wanamichezo kutoka Liverpool na klabu ya soka ya Chelsea.

