BAADA ya kutangazwa kuwa kocha Mkuu wa kikosi cha Simba Queens, Charles Lukula ameahidi kuwa hayupo kwenye timu kwa ajili ya kutalii bali kwa ajili ya kuisaidia timu hiyo kufanya vizuri kwenye michuano yote watakayoshiriki.

Lukula alitangazwa jana jumatatu akichukua nafasi ya aliyekuwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho Sebastian Mkomwa.

Akizungumzia mipango yake, Lukula alisema: “Nawashukuru sana viongozi kwa kunipa nafasi hii na mimi nitaifanyia kazi kwani sijaja kutembea.

“Mipango yangu ni kuisaidia timu kupiga hatua kubwa kwenye ligi ya mabingwa Afrika kwani Simba Queens ina wachezaji wazuri hivyo nitashirikiana na hao ambao nimewakuta.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa