KIKOSI cha Simba chini ya Kocha Mkuu, Juma Mgunda kimeanza mazoezi leo jumanne kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa hatua ya awali ya michuano ya Klabu bingwa Afrika dhidi ya De Agosto.

Katika mchezo huo Simba wataanzia ugenini mtanange utakaopigwa Oktoba 9 mwaka huu nchini Angola.

Akizungumzia maandalizi yao, Ofisa Habari wa Simba, Ahmed Ally amesema: “Kikosi kimerejea kambini leo jumanne tayari kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wetu wa ligi ya mabingwa Afrika dhidi ya De Agosto.

“Wachezaji wote wapo fiti baada ya mchezo wetu na Dodoma Jiji tunashukuru hakuna aliyepata majeraha hivyo wote watakuwa mazoezini kujiandaa na mchezo huo.

“Timu itaondoka Oktoba 8 kuelekea nchini Angola ambapo tutafika siku hiyo na baada ya mechi timu itaondoka kurejea Dar kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano.

“Tunawaomba mashabiki wetu wakati tunaporejea Dar kwa ajili ya mchezo wa marudiano wajitokeze kwa wingi kwani malengo yetu ni kuhakikisha tunaingia kwenye hatua ya makundi kwa kumtoa De Agosto.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa