UONGOZI wa klabu ya Polisi Tanzania, umelamba dili la Milioni 50 kutoka kampuni ya maji ya Jordan ambayo yanamilikiwa na Nabii, Clear Malisa.

Maji hayo yatatumiwa na wachezaji pamoja na viongozi wa Polisi Tanzania katika mazoezi, safari na mechi pia kwenye vikao vya viongozi mbalimbali wa timu.

Akizungumzia mkataba huo uliosainiwa Jijini Dodoma leo, Ofisa Habari wa Polisi Tanzania, Hassan Juma amesema kuwa “Ni kweli tumeingia mkataba na kampuni ya maji ya Jordan.

“Tunamshukuru sana kiongozi wa kampuni hiyo kwa kutupa udhamini huo mnono ambao utaisaidia timu na idara ya Habari pia.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa