Klabu ya Liverpool imeikataa ofa ya pili ya pauni milioni 30 iliyotolewa na Bayern Munich kwa Sadio Mane wakidai kwamba dau hilo halitoshi.

The Reds wameshangaa baada ya klabu hiyo ya Ujerumani kurejea tena na ofa hiyo baada ya ofa ya awali, iliyoripotiwa kuwa na thamani ya hadi £25m, kukataliwa.

Liverpool ambao wameanza harakati zao za kuinasa saini ya fowadi wa Benfica Darwin Nunez kwa dau la (£68.4m) wakati klabu hiyo ya Ureno inaripotiwa kutaka kiasi cha euro milioni 100 kwa mshambuliaji huyo wa miaka 22.

Liverpool wataka zaidi ya pauni ni milioni 40 kwa Mane ambaye alikuwa mchezaji muhimu kwenye mafanikio ya Reds msimu ulioisha wakifanikiwa kutwaa mataji mawili FA Cup na Carabao Cup lakini pia kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa na kumaliza katika nafasi ya pili kwenye EPL.

Bayern wanapambana kutafuta mbadala wa mshambuliaji Robert Lewandowski ambaye ameimbia miamba hao wa Bundesliga kwamba anataka kuondoka wakati wa dirisha hili la usajili.


Bila shaka unatamani ushindi mkubwa, vipi kuhusu kujaribu Sloti hii ya Aliya’s Wishes? jaribu ushinde sasa. Kasino ya Mtandaoni

CHEZA SASA

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa