Kocha mkuu wa Juventus Andrea Pirlo amesema mabingwa hao wanaoshikiria ubingwa wa Serie A lazima wajifunze kushinda bila uwepo wa Christiano Ronaldo baada ya supastaa huyo kuukosa mchezo wa Jumamosi dhidi ya Benevento.

 

Pirlo: Juventus Wajifunze Kushinda Bila Ronaldo.

Ronaldo alipumzishwa wikendi hii na juve ilishindwa kufanya vizuri kwa kulazimishwa sare ya 1-1 Juve walipokuwa ugenini.

Goli la ufunguzi la Alvaro Morata dakika ya 21 ya mchezo lilisawazishwa dakika ya 45 na mchezaji wa Benevento Gaetano Letizia kabla ya mchezaji huyo hajatolewa.

Juventus wapo nyuma ya viongozi wa Serie A kwa tofauti ya alama tatu na pirlo hajafurahishwa na kiwango cha wachezaji wake na amewataka kuimarika hata bila uwepo wa Ronaldo – ambaye amefunga magoli nane katika michezo mitano ya Serie A msimu huu.

“Ronaldo nimchezaji muhimu sana, sio tu kwetu sisi,” Pirlo aliongea na maripota baada ya mechi.

“Alikuwa ana umuhimu hata katika klabu ya Real Madrid.

“Aina hii ya mchezaji ambaye anafikia malengo, lakini lazima tujifunze kufanya vizri hata bila uwepo wake.

Juve wameshinda mchezo mmoja pekee katika michezo tisa ya ugenini kwenye Serie A.

Wababe hao wa Italia ambao wameshinda mechi nne na kutoa sare tano, na wamefikia idadi ya michezo waliyotoa sare msimu uliyopita pia ameirudia rekodi ya mwaka 2001-02 kutoa sare tano katika mechi tisa.

“Siogopi, lakini lazima tufikirie kwamba michezo inaendelea na tayari tumepoteza alama nyingi.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

16 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa