Eden Hazard anasumbuliwa na jeraha lililopelekea kutolewa nje kwenye mchezo wa Jumamosi ambapo Real Madrid ilipoteza kwa 2-1 dhidi ya Diportivo Alaves.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Belgium amekuwa akisumbuliwa na tatizo la kifundo cha mguu na miguu tangu ajiunge na timu ya Zinedine Zidane akitokea katika klabu ya Chelsea miezi 18 iliyopita.

Hikuwekwa wazi ni jeraha la sehemu gani alilopata siku ya Jumamosi, baada ya kutoka katika dimba la Alfredo Di Stefano, nafasi yake ilichukuliwa na Rodrygo baada ya Hazard kutumia dakika 28 pekee.

Hazard alidondoshwa katika eneo la penati katika lango Alaves mapema wakati wa mechi hiyo lakini mwamuzi alisema kulikuwa hakuna faulo.

Alionekana kuinama na kujishika mguuni na ilionesha alikuwa kwenye maumivu makali.

Ulikuwa mchezo wake wa tatu wa LaLiga kwa msimu huu baada ya kucheza michezo miwili dhidi ya Villarreal na Huesca.

Msimu uliyopita Hazard alianza katika michezo 14 katika ligi ya LaLiga alitumika kidogo na Madrid walifanikiwa kushinda taji la LaLiga ikiwa ndiyo msimu wake wa kwanza katika klabu hiyo.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

14 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa