Lionel Messi ametoa mchango wake kwa Diego Maradona siku ya Jumapili wakati akishangilia goli jambo alilofanya kama “Surprise nzuri” kwa wachezaji wenzake wa Barcelona.

Messi Amuenzi Maradona kwa Mtindo Wake.

Mchezaji wa zamani wa Barcelona na timu ya taifa ya Argentina Maradona alifariki siku ya Jumatano akiwa na umri wa miaka 60 na alitolewa heshima kabla michezo yote ya LaLiga haijaanza wikendi hii.

Messi aliifungia timu yake goli la nne katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Osasuna na baada ya kufunga alivua tisheti yake ya Barca na kubaki na jezi ya Newell’s Old Boys klabu yake ya utotoni ambayo pia ni jezi aliyokuwa akivaa Maradona 1993-94.

Pia alionesha ishara ya saluti mawinguni kama heshima kwa mataifa mwenzake, ambaye alitumia msimu na klabu hiyo ya Newell’s ambako Messi alianza kucheza soka.

Antoine Griezmann na Philippe Coutinho wote walifunga katika ushindi mnono wa Barca pamoja na Martin Braithwaite ambaye alifunga goli la kwanza katika kipindi cha kwanza.

Walielezea kwamba walikuwa hawajui kitu ambacho Messi alikipanga siku ya leo katika dimba la Camp Nou ambako Maradona alicheza kutoka mwaka 1982-1984.

“Tumempoteza Maradona, kioo cha wachezaji wengi ulimwenguni tutamkumbuka sana,” Coutinho alisema.

“Hatukujua kama Messi amejiandaa kuonesha heshima kwa Maradona,” alisema Griezmann “Ilikuwa zawadi nzuri.”

Ushindi wa Barca unawasogeza mapa nafasi ya nane katika jedwali la LaLiga alama tisa nyuma ya viongozi wa ligi hiyo Real Sociedad.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa