Edinson Cavani ameonesha kiwango kikubwa kwa kuokoa jahazi la Manchester United kutoka nyuma kwa goli mbili mpaka kushinda kwa 3-2.

Goli la kichwa la Jan Bednarek na goli la free-kick la Ward-Prowse yaliiweka mbele Southampaton kipindi cha kwanza katika dimba la St Mary’s Stadium.

Lakini ujio wa Edinson Cavani katika kipindi cha pili ulidhihirisha Ole Gunnar Solskjaer alikuwa na akiba ya silaha muhimu katika dakika ya 59 ya mchezo alio mpasia pasi safi Bruno Fernandes ambaye alifunga goli la kwanza kwa Man United.

Kisha akakutana na shuti ambalo lilimbabatiza mchezaji wa Soton na kufunga kwa kichwa goli lililofanya ubao wa matokeo kusoma 2-2, katika muda wa nyongeza akaweka kambani goli la tatu dakika ya 92 na kuifanya Man United kupata ushindi wa nane mfululizo ugenini katika Premier League.

Manchester United amesogea mpaka nafasi ya nane katika msimamo wa Premier League akiwa amekamata alama 16 sawa na Everton lakini United anamchezo mkononi.


USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa