Mchezaji wa zamani wa Fulham, Portsmouth na timu ya taifa ya Senegal – Papa Bouba Diop amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 42.

Diop aliwahi kuvitumikia vilabu mbalimbali vya EPL ikiwemo West Ham United na Birmingham City na alicheza jumla ya michezo 129.

Mashabiki wa Senegal watamkumbuka Papa Bouba Diop kwa kufunga goli la pekee katika mchezo dhidi ya Ufaransa katika mashindano ya Kombe la Dunia mwaka 2002.

Papa Bouba Diop, Papa Bouba Diop Afariki Dunia., Meridianbet
Diop Alipokuwa akiitumikia West Ham United.

Kupitia ukurasa wa Fifa, imeandikwa “Uliwahi kuwashujaa wa Kombe la Dunia, utabaki kuwa shujaa wa Kombe la Dunia.”

Ukurasa wa twitter wa timu ya Fulham wameandika ” klabu inahuzunika. Pumzika kwa amani Wardrobe”

Papa Bouba Diop, Papa Bouba Diop Afariki Dunia., Meridianbet
Diop Alipokuwa akiitumikia timu ya Taifa ya Senegal.

Diop aliisaidia Senegal kufika hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Dunia 2002 na alicheza mashindano ya Afcon mara 4 yakiwemo mashindano ya mwaka 2002 ambapo Senegal walimaliza nafasi ya pili na mwaka 2013, Papa Bouba Diop alistaafu kucheza soka.

Rais wa Senegal  – Macky Sall amesema “kifo cha Diop ni pengo kubwa kwa Senegal.”


FURAHIA MUZIKI MTANDAONI HUKU UKITENGEZA MKWANJA!!

Mchezo wa Astro Legend unakupatia burudani ya muziki kupitia kasino ya mtandaoni ya Meridianbet. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!

Papa Bouba Diop, Papa Bouba Diop Afariki Dunia., Meridianbet

INGIA MCHEZONI

11 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa