Tottenham : Sajili Zingine 5 Kufanyiwa Kazi

Ripoti zinataja Tottenham wanafanyia kazi angalau saini tano zaidi baada ya kumaliza kumnasa Pierre-Emile Hojbjerg kutoka Southampton.

Wana London hawa walitangaza kuwasili kwa Hojberg jana kwa ada ya £15millioni ambayo kuna uwezekano wa kuongezeka hadi pauni 19m.

Taarifa kutoka chanzo cha ndani ya klabu kinasema kuwa Spurs wanajiandaa kusajili wachezaji wengine 5 wapya wakati Jose Mourinho akijaribu kuboresha kikosi kabla ya kampeni mpya.

Mreno huyu anajaribu kusaini beki wa kulia, beki wa katikati, kiungo mshambuliaji, mshambuliaji anayeweza kufanya kazi popote kwenye safu ya ushambuliaji na kipa wa ziada.

Mourinho anatajwa kuwa tayari ameshaweka vipaumbele vyake tayari, na hilo ndiyo jema zaidi kwake, baada ya kutua Hojbjerg ambaye walikuwa wakimlenga kwa mda mrefu.

Lazima Tottenham Wauze ili Wanunue

Ili kufanya ununuzi mkubwa Tottenham wanapaswa kuuza. Wana hawa wa London wako kwenye mazungumzo ya kumuuza Serge Aurier, mchezaji anayetumai anaweza kuipa klabu angalau £20m baada ya £12m ya Kyle Walker-Peters.

Nyota wengine wanaotarajiwa kuondoka Tottenham wanaweza kuwa ni pamoja na mabeki Juan Foyth, Danny Rose na Cameron Carter-Vickers pamoja na kiungo mshambuliaji wa muda mrefu Erik Lamela.

Kuna uvumi kwamba Tanguy Ndombele pia ataondoka Spurs, ikiwa ni pamoja na uwezekano wa kuhusika kwenye mpango wa kubadilishana wachezaji ambao unaweza kuwaleta nyota kadhaa wakubwa pale Spurs.

Hata hivyo, klabu ya Tottenham imekuwa ikipuuza taarifa hizi na kutotaka kuzungumzia sana.


 

Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

Soma Zaidi

35 Komentara

    Vizuri kama wakiboresha kikosi chao ili waje walete ushindani

    Jibu

    Of a hivyo sasa kwa timu zisizo na mabeki kama Chelsea ni muda wenu sasa

    Jibu

    Safi!

    Jibu

    sio mbaya ili kuboresha kikosi msimu mpya

    Jibu

    Ni vizuri ili kuimarisha kikosi msimu ujao

    Jibu

    Spurs wanataka kutengeneza kikosi cha ushindani msimu ujao ni jambo zuri kwa wana spurs.

    Jibu

    Tunasubiri kuona wachezaji watakaosajiliwa

    Jibu

    Morinho anampango wa kutengeneza kikosi Cha Spurs ambacho kitakuja kuleta ushindani msimu ujao ni Jambo la furaha Sana kwa Wana Spurs.

    Jibu

    Tottenham wanajipanga kikamirifu ligi msimu hujao

    Jibu

    Msimu ujao Tottenham lazima watakuwa fiti sana

    Jibu

    Tottenham imeshiriki ligi ya mabingwa kwa misimu minne iliyopita na msimu ujao itakosa nafasi hiyo pengine usajiri mzuri utapelekea kurudi katika nafsi yake ya juu kwenye ligi ya EPL#meridianbettz

    Jibu

    Tunasubiri maajabu ya usajili huo msimu ujao

    Jibu

    Tunasubili tuone maajabu huo msimu ujao usajili utakuwaje#meridianbettz

    Jibu

    Kila la kheri Ila vigezo na masharti wazingatieh wasije wakakutwa na rungu la UEFA

    Jibu

    Ni vizuri kuboresha kikosi chao ili walete mabadiliko katika club yao

    Jibu

    Msimu ujao nijambo zuri wana spurs

    Jibu

    Imekaa poa tusubir tuone!!

    Jibu

    Muda wa kusajili viungo na kujipanga kikosi

    Jibu

    Habar njema

    Jibu

    Basi sawa

    Jibu

    Habari njema Sana

    Jibu

    We are waiting for this

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Safiiii tunasubir mabadiliko!!!!

    Jibu

    Iko vizur

    Jibu

    Ni vizuri kuimarisha kikosi
    @meridianbettz

    Jibu

    Hii ipo poa sana kwa tottenham na kocha wao kibuli

    Jibu

    Sasa ni wakati wa Mourinho kufanya yake kwenye usajiri

    Jibu

    Kikosi kitakuwa safi

    Jibu

    Aya sasa aweke sawa kikosi chake

    Jibu

    Tunasubili tuone.

    Jibu

    apo kocha wa spurs akiweka daau zuri zaidi atasajili wachezaji wazuri zaidi

    Jibu

    Kocha wa kukutupuka kashaanza kazi yake

    Jibu

    Wasuke suke tu watapata wachezaji wazuri

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.