Kocha wa klabu ya nchni Qatar Al Sadd, Xavi Hernandez amesisitiza kwamba anazingatia zaidi kazi yake na Al Sadd licha ya kuripotiwa anajipanga kuchukua mikoba ya kuwa kocha mkuu wa Barcelona.
Baada ya Ronald Koeman kufungishwa vilago siku ya Jumatano baada ya kupokea kichapo cha 1-0 kutoka kwa Rayo Vallecano kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2002 imewafanya The Blaugrana kuachwa alama tisa kutoka kwa viongozi wa LaLiga Real Sociedad.
Alipoulizwa juu ya uwezekano wa kurejea Camp Nou kama kocha mkuu siku ya Alhamisi Xavi alisema: “Ninazingatia kazi yangu na Al Sadd na siwezi kuongea chochote kile.”
Xavi aliweza kufunga mabao 85 na kutoa asisti 184 katika michezo 767 alipokuwa mchezaji wa Barcelona.
Barca wanajiandaa na mchezo wa Jumamosi dhidi ya Alaves wakiwa chini ya kocha wa muda Sergi Barjuan vilevile watakuwa na mechi ya Ligi ya Mabingwa siku tatu badaye.
Mchongo wa mkwanja mrefu kutoka kasino bora za mtandaoni za Meridianbet. Mchezo wa Circus Fever unakuweka katika nafasi nzuri ya kuwa mshindi. Furahia kasino maridhawa kutoka nyumba ya mabingwa meridianbettz.

CHEZA HAPA

