Zahera: Simba Ina Bahati

KOCHA Mkuu wa zamani wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa katika timu nne zinazoshiriki michuano ya kimataifa kwa msimu huu, Simba pekee ndio yenye bahati.

Timu nne ambazo zinaiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya kimataifa mpaka sasa ni pamoja na Simba, Yanga, Azam na Kipanga FC kutoka Zanzibar.

Akizungumzia michezo ya marudiano ya timu hizo, Zahera amesema Simba ina bahati katika michuano hiyo baada ya kupata matokeo hivyo itakuwa kazi rahisi kwao kuvuka hatua ya makundi.

“Kwa wakati huu hakuna timu ndogo kwenye haya mashindano kwani yeyote anaweza kupata nafasi ya kusonga mbele na kila timu ina bahati.

“Lakini kwa upande wangu Simba ana bahati ya kuvuka kwenda kwenye hatua ya makundi kutokana na matokeo aliyopata ila wanapaswa kupambana kwani lolote linaweza kutokea.”

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.