Mkurugenzi wa zamani wa klabu ya Ajax Marc Overmars amechaguliwa kuwa mkurugenzi mpya wa ufundi kwenye klabu ya Ubelgiji ya Antwerp ni mwezi tu baaada ya kujiudhuru kazi kwenye klabu ya Ajax kwa tabia mbovu alionyesha kwa moja ya wafanyakazi wa kike.

Marc Overmars aliwai kuchezea vilabu vya Arsenal na Barcelona, mwezi uliosha ghafla aliachia ngazi kwenye klabu ya Ajax, baada ya kukubali kufanya tabia zisizofaa ndani ya klabu kwa kuwatumia jumbe na picha wanawake aliokuwa akifanya nao kazi.

Marc Overmars

Kwenye utambaulisho wake kwenye klabu hiyo mpya Overmars alisema swala la Ajax limeshughulikiwa vizuri na halijaathili mazungumzo na mwajili wake mpya.

“Kilichotokea Ajax hakitatokea tena,” alinukuliwa na kituo cha habari nchini Ubelgiji.

“Nina furaha kuwa hapa, ni ukurasa npya kwangu, na ni changamoto nzuri kwa klabu ambayo ina fursa ya kukua.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa