Man United Wavutiwa na Richarlison

Klabu ya Manchester United wanataka kuimarisha eneo la ushambuliaji na inavutiwa zaidi na kumsajili mchezaji wa Brazil Richarlson.

Man United Wavutiwa na Richarlison

Mashetani Wekundu wamekuwa na uhaba wa mabao mengi msimu huu ingawa wachezaji kama Jadon Sancho ni kama tayari wamejipata lakini tatizo limekuwa eneo la mbele.

Richarlson ambaye anaichezea Everton ambao wanapambana kuepuka kushuka daraja msimu huu ameifungia klabu hiyo yas EPL mabao 42 tangu aliposajiliwa mwaka 2018 kwa £35m akitokea Watford.

Kocha wa muda wa United Ralf Rangnick anajiandaa kuachia nafasi hiyo mwishoni mwa msimu huu na aliwahi kusema kwamba klabu inahitaji kupata fowadi mwingine sababu mkataba wa Cavani unaelekea mwisho na Ronaldo anaelekea ukingoni mwa kazi yake.

Carlo Ancelotti kocha wa Real Madrid pia aliwahi kuhusishwa kuitaka huduma ya Mbrazili huyo ambaye aliwahi kufanya naye kazi wakati akiinoa Everton kabla ya kuajiriwa na Los Blancos.


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

Acha ujumbe