Feitoto Amkimbiza Chama kwa Takwimu

Takwimu zilizopo kwa sasa kwa viungo wa timu mahasimu wa jadi Bongo Simba na Yanga, Feisal Salumu (Feitoto) wa Yanga na Clatous Chama wa Simba zipo tofauti tangu kuanza kwa msimu huu na Chama anaonekana kusubiri kidogo kwa Fei.
Feisal tangu kuanza kwa msimu huu wa 2022-23, ameonekana kuwa moto zaidi kuliko Chama akiwa amehusika kwenye kuisaidia Yanga kupata ushindi au alama kwenye mechi zote tofauti kabisa na ilivyo kwa mwamba wa Lusaka.

Feisal ameshacheza dakika 720 ambayo ni sawa na mechi nane, akiwa amefunga mabao manne, akiwa hana pasi hata moja ya bao (assist). Jumla amekuwa amehusika kwenye magoli manne hadi sasa kwenye ligi hii.

Chama akiwa na Simba msimu huu amecheza pia mechi nane, sawa na dakika 720.

Amefunga bao moja pekee, akiwa amehusika kwenye pasi mbili za magoli (assit) na kumfanya kuwa uhusika wa mabao matatu kwenye mechi nane za msimu huu.

Kwa mabao hayo ya Feisali imeweza kuipaisha Yanga kufika kwenye kilele cha ligi wakiwa na alama 20 na kutengeneza rekodi ya un-beaten kwenye mechi 45 za ligi kuu. Wakati Chama kabla ya mechi ya jana dhidi ya Mtibwa Simba ilikuwa kwenye nafasi ya nne na pointi zake 14.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.