Baada ya kupoteza mchezo dhidi ya Kagera Sugar, Kocha Mkuu wa kikosi cha KMC, Thierry Hitimana amempa lawama zote kipa wao, Adjiguesena Balora.
Mchezo huo wa ligi kuu ulipigwa jana kwenye Uwanja wa CCM Kirumba ambapo Anuary Jabir ndiye aliifungia Kagera Sugar bao pekee la ushindi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Hitimana alisema makosa ya kwenye mchezo huo yamefanywa na kipa wao.
“Kwanza tunamshukuru Mungu mchezo umemalizika salama, kikubwa tumetengeneza nafasi nyingi lakini tukashindwa kuzitumia ila wenzetu wametengeneza moja wameitumia.
“Ni kama mchezo wa tatu sasa tunapoteza kwa makosa binafsi ya kipa na kusababisha kupoteza mchezo hivyo naona shida kubwa ipo kwenye eneo hilo.
“Tunaendelea kubaki Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mchezo mwingine wa ligi, tutaenda kufanya marekebisho mbalimbali yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo.”

