MAUYA KUWAKOSA BELOUZDAD

Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Ally Kamwe ameweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa kesho dhidi ya CR Belouizdad wa Ligi ya Mabingwa Afrika ni Zawadi Mauya pekee ndio hayupo katika mpango wa mchezo huo wa kesho.

Nyota huyo aliumia kwenye mchezo wa michuano ya Azam Sports Federation Cup dhidi ya Polisi Tanzania.

Hivyo, Madaktari wamethibitisha yeye pekee ndiye hadi Sasa ameshindwa kurejea kwenye afya yake kiasi cha kuweza kutumika kwenye mchezo huo Muhimu.

“Mpaka sasa, ni Zawadi Mauya pekee ambaye atakosekana kwenye mchezo wetu. Alipata majeraha kwenye mchezo wetu wa FA dhidi ya Polisi Tanzania na Sasa anajiuguza,” alisema.

Acha ujumbe