Beki kisiki wa Bayern Munich, David Alaba amethibitisha kuwa ataondoka katika klabu hiyo ya Bavaria mwishoni mwa msimu huu.
David Alaba amethibitisha kuwa ataondoka Bayern Munich mwishoni mwa msimu baada ya kuwepo klabuni hapo kwa takribani miaka 13.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 ataondoka Allianz Arena kwa uhamisho wa bure mara tu mkataba wake na mabingwa wa Bundesliga utakapomalizika mnamo Juni.
Real Madrid, Chelsea na Liverpool zote zimehusishwa kumsajili beki huyo, lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Austria bado hajasema anapoelekea.
Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari ambao haukupangwa, Alaba alisema: “Nimefanya uamuzi wa kuondoka Bayern mwishoni mwa msimu huu na kujaribu kitu kipya.
Ni wazi haukuwa uamuzi rahisi, nimekuwa hapa kwa miaka 13 na klabu hii imekuwa kila kitu kwangu, hivyo ninashukuru kwa mengi sana na ndio sababu nasema uamuzi huu kwangu umekuwa mgumu sana. Ninaweza kusema Bayern ni familia yangu.” aliongeza Alaba.
Treasure Heroes inakupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!
Angelina
Nice update
Mwanahamisi
Safi
Lydia Emmanuel Magoti
Safii
Neema juma
Sio mbaya ni jambooo la kheri pia
Hopemwaikuka
All ze best to him
Sarah
Safii
Dorophina
Alaba haende tu liverpool
Caroline
Apambaneee
Rahma
Nice
Adelta
Ni sawa tu
Sadick
Alaba ameiga mfano wa Thiago Alcantara aliyeamua kuondoka Bayern Munich. Bayern Munich inatakiwa kusajiri msimu ujao.
warda
Angekuja Man U jamani