Alexis Sanchez Alitaka Kuondoka United

Aliyekuwa nyota wa Man United, Alexis Sanchez alitaka kuondoka Manchester United mapema kabisa, baada ya mkataba wake na Manchester City kushindwa kufanya kazi.

Januari 2018, Manchester City walikuwa wanatarajia kumsajili Sanchez akitokea kwa washika mtutu Arsenal, lakini dili lilienda kuwa tofauti kabisa na akajikuta ametimba kwa wapinzani wao Man United kwa dili la mabadilishano na Henrikh Mkhitaryan.

Nyota huyu alipofika Man United alishindwa kuonesha ubora ule ule aliokuwa nao alikotoa, ambako alichukuliwa kama miuongoni mwa washambuliaji wa kali zaidi wa ligi ya Uingereza. Alikuwa analipwa £390,000 kwa wiki.

Katika mechi 45 alizocheza na United aliambulia magoli 5 tu! Tofauti na ambavyo wengi walitarajia, kisha akapelekwa Inter Milan kwa mkopo msimu wa 2019-20, kabla hawajakamilisha dili la kudumu katika dirisha hili la uhamisho.

Nyota huyu alikuwa akipata shida ya majeraha, lakini anabainisha kuwa hakujiona akifurahia mazingira ya Manchester United tangia awali kabisa.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Alexis Sanchez aliamua kuweka bayana baadhi ya mambo ambayo anaamini mashabiki na wapenzi wa soka walikuwa hawayafahamu alipokuwepo United. Na pengine mambo hayo yalimfanya aonekane mbaya.

Chaguo la kwanza la Alexis Sanchez ilikuwa ni Manchester City

Sanchez alitamani zaidi kuwepo Manchester City. Licha ya kujikuta tayari alikuwa ameshatua United, ameyasema haya ya moyoni;

“Kabla ya kwenda kule [United] nilikuwa na makubaliano na Manchester City, lakini hii haikwenda sawa na nikapata nafasi ya kujiunga na Manchester United. Ilikuwa kitu kizuri ni klabu niliyoipenda nikiwa mtoto. Hatimaye nilisaini bila kuuliza nini kinatokea ndani ya klabu.”

“Kuna mambo ambayo hauwezi kuelewa mpaka uwepo pale, nilielewa mengi siku ya kwanza nilipokuwa mazoezini.” -Alexis Sanchez

Alexis Sanchez anasema kuwa aliwaambia familia yake na wakala kuwa hakuna uwezekano wa kurejea Arsenal? na ikachukuliwa kama utani. lakini hakufurahia kadri siku zilivyosonga. Alitaka aondoke.


 

SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

 

 

 

33 Komentara

    Siku nyngne utulize akili zako ili uwe na aman ya moyo

    Jibu

    Duu hii kaliii

    Jibu

    Mambo ya soka hayo!!!

    Jibu

    Duuuh hatarii

    Jibu

    Asichukue maamuzi Kwanza atulie

    Jibu

    Sanchez united hakuitendea haki

    Jibu

    Afikiri kabla ya kutenda

    Jibu

    Sanchez hakuna chochote alicho kitendea man u Ni bora haende tu kama anataka kuondoka hana mchango wowote kama klabu ilivyofikilia kwamba atakuwa na msaada

    Jibu

    sanchez nae aache tamaa atulie apo alipo panamfaa

    Jibu

    Duh noma sana hiii

    Jibu

    Mara nyingi changamoto kama hizi wachezaji wengi wamekuwa wakikutana nazo hasa pale wapotoka kwenye timu moja kwenda nyingine ila kiukweli mbali na yote haya Sanchez hakuwa na msimu mzuri Old Trafford huenda ikawa imechangiwa na kukosa furaha

    Jibu

    Ni kweli Alexis Sanchez amekutana na changamoto bora aondoke tu@meridianbettz

    Jibu

    Changamoto kubwa

    Jibu

    wahenga walisema fikiria kabla hujatenda ona sasa yaliyomkuta sanchez

    Jibu

    Changamoto sanaa

    Jibu

    Alex kapata Sana majeraha msimu uliopita

    Jibu

    Sanchez nae alitaka kuondoka man u ndio maana akucheza vizuri

    Jibu

    Changamoto kubwa

    Jibu

    Duuh Mambo ya soka ayo yametaladadi#Meridianbettz

    Jibu

    asante meridianbet kwa habar moto moto

    Jibu

    Nyota huyu alipofika Man United alishindwa kuonesha ubora ule ule aliokuwa nao alikotoa, ambako alichukuliwa kama miuongoni mwa washambuliaji wa kali zaidi wa ligi ya Uingereza. Alikuwa analipwa £390,000 kwa wiki.

    Jibu

    Duuh majanga hayo endelea tuu hapo hapo

    Jibu

    Atulie tu man u

    Jibu

    Kipige tuu Man U panakufaa krabu kubwa iyo pambana Napo hapo hapo

    Jibu

    Kwa style ya United Sanchez pale haikua sehem sahii

    Jibu

    Sanchez alitamani zaidi kuwepo Manchester City. Licha ya kujikuta tayari alikuwa ameshatua United, ameyasema haya ya moyoni;

    Jibu

    Maneno hayo yanamaanisha alipoteza imani mara baada ya kujiunga Man U pengine ndio maana hakupata mafanikio#meridianbettz

    Jibu

    Sanchez united hakuitendea haki

    Jibu

    Hatari#meridianbettz

    Jibu

    Acha asepe tu

    Jibu

    Mmh

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.