Kiungo wa zamani wa Real Madrid Carlos Casimiro (30), amewaaga mashabiki zake pamoja na timu yake hiyo ya Madrid, huku akitarajia kuanza Maisha mapya ya soka jijini Manchester baada ya usajili wake kukamilika.

casemiro,  Casemiro Aaga Madrid Asema Atarejea Tena., Meridianbet

Manchester United wamemsajili kiungo huyo raia wa Brazil, kwa dau la Euro Milioni 70 ili kuimarisha kikosi chao, baada ya kuona mapungufu kwenye baadhi ya maeneo ikiwemo eneo la kiungo.

casemiro,  Casemiro Aaga Madrid Asema Atarejea Tena., Meridianbet

Kupitia ukurasa wake wa Twitter ameandika taarifa yake ya kuaga kwa lugha ya kihispania akimaanisha kwamba:

Nimeishi ndoto nzuri sana ambayo nimewahi kufikiria. Natumai nitarudi siku moja sehemu ambayo itakuwa nyumbani kwangu kila wakati. Si katika maisha elfu moja nitaweza kurudisha yale yote Real Madrid mliyonipatia. Hala Madrid! Daima!

Mashabiki wa Casemiro wameonekana kumtakia kila la heri katika Maisha yake mapya ya soka huku baadhi pia wakikumbushia matukio mengi aliyowahi kuyafanya akiwa Madrid.

Ronaldo

Na sasa Casemiro ataenda kuungana na wachezaji wenzake aliowahi kucheza nao akiwa Madrid kwa misimu mingi Cristiano Ronaldo, na Varane.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa