Wakati huu ambao msimu umemalizika na wachezaji wengi kuwa likizo, klabu ya Chelsea bado inakazi ya kufanya. Muda unakwenda, mambo hayaeleweki.

Mchakato wa kukamilisha uuzwaji wa Chelsea bado ni changamoto, licha ya wamiliki watarajiwa kusaini mikataba na The Blues, kuna changamoto kubwa kwenye upande wa utawala hasa kwa mmiliki anayetoka, Roman Abramovic.

Japokuwa anatambulika kama raia wa Urusi, Abramovic anamiliki pasipoti ya Ureno na hivyo, ili serikali ya Uingereza iweke kukamilisha mchakato wa uuzwaji wa Chelsea, inapaswa kupewa kibali cha mchakato huko na serikali ya Ureno.

Sasa hapa sio shida ya Ureno na Uingereza, hapa kunasiasa za Uingereza na Umoja wa Ulaya. Uingereza alishajitoa kwenye Umoja wa Ulaya na kwa siku za hivi karibuni, wanapata shida kwenye mazingira ya mashirikiano na nchi wanachama wa Umoja huo.

Chelsea, Chelsea Watatoboa UEFA Msimu Ujao?, Meridianbet
Roman Abramovich

Wakati hilo likiendelea nyuma ya pazia, uongozi wa EPL unatarajia kupeleka mapendekezo ya timu kutoka kwenye ligi hiyo zitakazocheza mashindano ya Ligi ya Mabingwa (UEFA) msimu ujao.

Pamoja na hilo, EPL inatarajia kutoa leseni kwa vilabu vitakavyoshiriki ligi hiyo mapema Juni 9, 2022. Vilabu vitakavyohusika kwenye mchakato huu ni vile vyenye leseni ya soka ya muda mrefu, The Blues hawapo kwenye kundi hili.

Chelsea, Chelsea Watatoboa UEFA Msimu Ujao?, Meridianbet
Msimamo wa EPL, 2021/22.

Kama kufikia Mei 30, 2022 (ambapo ndio ukomo wa leseni maalumu waliyopewa Chelsea na serikali ya Uingereza) klabu hiyo itakua haijakamilisha mchakato wa kuuzwa na kupatiwa leseni kama vilabu vingine, kuna uwezekano mkubwa ikakosa nafasi ya kupendekezwa kwenye UEFA na pengine ikakosa nafasi ya kucheza EPL msimu ujao mpaka pale sakata lao litakapotatuliwa kwa ufasaha.

Ikitokea The Blues hawachezi UEFA, nafasi yao itakwenda moja kwa moja kwa Arsenal ambao wamemaliza katika nafasi ya 5 kwenye msimamo wa EPL msimu huu.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa