Nyota Christian Eriksen amebainisha kuwa kinachoendelea kwake Inter Milan ‘sio kile alichokiota’ na yuko tayari kwa uhamisho wa dirisha la Januari ikiwa hatapewa mda zaidi wa kucheza.
Kiungo huyo ambaye yupo kwenye jukumu la kitaifa na Denmark, alizungumza na TV2 Sport juu ya kutokuwa na mchango mkubwa chini ya Antonio Conte.
“Hapana, hiki sio kile nilichokiota,” alikiri nyota huyo wa zamani wa Tottenham Hotspur.
“Nadhani wachezaji wote wanataka kucheza kadri inavyowezekana, lakini mwishowe kocha anaamua ni nani atakayeingia uwanjani.”
“Ni hali kubwa ya kushangaza, kwani mashabiki wanataka kuniona nikicheza zaidi na mimi pia, lakini kocha ana maoni tofauti na kama mchezaji lazima niheshimu hilo.” – Christian Eriksen
Christian Eriksen anasema kuwa kimsingi, Inter kwa sasa mambo hayaendi, lakini pia anakubali kuwa alipokuwa nje ya timu ilikuwa inapata ushindi, lakini hii haimaanishi uwepo wake ndiyo unaikwamisha timu kwa sasa.
Lakini, hakujaribu kuficha uwezekano wa kuondoka Januari, wakati PSG wakitajwa kuwa inavutiwa na huduma yake.
“Kwa sasa, ninazingatia soka langu tu, kisha tutaona wakati dirisha la uhamisho likifunguliwa ikiwa kuna jambo litatokea au la.” – Christian Eriksen
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!
Hopemwaikuka
Sio kila unachokiota lazima kiwe vile vile so relax
Zeiyana
Inaoneka kocha hajapendekezwa na kazi yake Eriksen na ndio maana hamekua hampi number kwenye kikosi ukiangalia wachezaji wengi sana chipukizi mwenye umli mdogo tu ukiachiliana mbali na humri halio kua nao
Elika
Awe mpole tu
Khadija
Atulie tu
Lydia Emmanuel Magoti
Kuwa na subila jembe ndoto zako Zita timia
Dorophina
Inabidi aheshimu maamuzi ya kocha atulie tu
magdalena
eriksen alikuwa na matarajio makubwa sana ilaa anaona yanaenda sivyo
Adelta
Huwezi kuota ndoto ikatimia yote nyingine .huishia njiani kwa hiyo awe tu mpole
ester jackson
Uko sahihi kabisa kwa upande mwingine tunawatupia lawama makocha ila kwa vingine nasema kuwa kama shirika la michezo la upande wa mpira wa mguu wangeweka idadi ya kubadili wachezaji 5 kama mwanzo ingekuwa vizuri mana wachezaji wengi wangepata nafasi lakini ni 3 tu inabidi lawama tuwape wengine kocha huwa anatimiza jukumu lake tu na wachezaji wote wanapenda kucheza mpira
Sadick
Eriksen alitaka changamoto mpya, nadhani hiki ndicho alichohitaji nacho ni kupigania namba
Fatina mfigi
Subira yavuta kher
Povel
Erikson alifany makosa makubwa sana kuondoka spurs ilibid ajaribu kuangaliah upepo jinsi ulivyo sasa noana mambo yanazid kwenda kombo ndani ya milan naiman czan Kama January ataendeleah kusaliah milan
Tatu
Erikson anandoto ya kufika mbali sasa kocha wake anamuweka benchi sana
Mwajumah
Awe mpole tu
Issa
Eriksen anajua kazi yake intet. Imepata mtu
Sabrina
Inabidi awe mpole kwanza
Sauda
Avute subira
Carolyn
Erikson alifanya makosa makubwa kuondoka totenham
Angelina
Goodupdate
Rahma
Itabidi tu awe mpole
aisha
Inter imepata kiingo fundi na amekua kwenye kiwango bora toka msimu wa mwisho alivyokiwa totenham
Saupha mohamed
Atutulie