Toni Kroos anaamini Zinedine Zidane atairejesha Real Madrid katika kiwango kama alivyowahi kufanya kipindi cha nyuma.
Mabingwa watetezi wa LaLiga waliuanza msimu kiugumu wameshinda mechi sita kati ya 11 kwenye mashindano yote.

Kulikuwa na mshituko wa kupoteza mfululizo katika dimba la nyumbani dhidi ya Cadiz na Shakhtar Donetsk, Los Blancos ilipokea kichapo cha 4-1 kutoka kwa Valencia kabla ya kwenda mapumziko kwaajili ya michezo ya kimataifa.
Madrid ilipata ushindi mnono dhidi ya mahasimu wao Barcelona pia ilishinda dhidi ya Inter katika Champions League na kiungo Kroos amesema muendelezo wa ushindi imekuwa changamoto kubwa.
“Ni kweli tunakosa kitu fulani, sio siri kila mtu anaweza kuona,” aliiambia Marca “Tunatakiwa kuwa na muendelezo.
“Kma ukiangalia matokeo, mawili mazuri mabaya moja , mazuri mawili mabaya moja, tuna hitaji kuwa bora.
“Kama tuliwafunga Barcelona basi pia tulipaswa kufanya hivyo dhidi ya Cadiz na Shakhtar nyumbani.
Zidane aliwajibika kwenye mchezo dhidi ya Valencia, kwa mara ya kwanza Madrid imeruhusu magoli manne kwenye mchezo wa ligi tangu mchezo wa Clasico ambapo Madrid ilipoteza kwa 5-1 Oktoba 2018 na ili gharimu kazi ya Julen Lopetegui
“Anajua ndani ya Madrid usipo kuwa na matokeo na usipo timiza matarajio basi mazungumzo hufanyika,” Kroos alisema. “Hiyo ndiyo maana tupo katika klabu hii ni kawaida.
Mwisho ya yote tulicho bakiza ni kuimarika na kujaribu kushinda michezo yetu, kocha tatafuta njia ya kumaliza tatizo.
Jaribu sasa hapa Meridianbet. Ukiacha ukweli kuwa itakupa burudani maridadi, bado inakuhakikishia ushindi mkubwa. Kazi kwako kukusanya ushindi!



Hopemwaikuka
Inawezekana tu akiwa na nia na juhudi
Dorophina
Zidane anambinu nyingi za kufundisha atairudisha tu madrid ilipotoka
Lydia Emmanuel Magoti
Itakuwa vizuri Zidane auwashe moto kwa mwenendo mwingine
Fatina mfigi
Itakuwa Ni vizur akirud kwenye ubora wake!
magdalena
inawezekana ikawa ivyo sanbabu zidane yupo makini sana
Povel
Inawezekana Kama watafany usajil katika maeneo wanayoona yanamapungufu co Kama watafany hvy hata mm naiman anawez kurud kwny ubora tuliouzoeh Kama mara kwanza kocha zizzou
ester jackson
Inawezekana kama watafanya usajili mzuri January
zeiyana
Zidane haangalie wapi alipo kosea
Tatu
Zidane akipewa mda real madrid wanaweza kuludi kwenye hali yake
Adelta
Zidane aongeze juhudi
Nasra
Aongeze juhudi
Mwajumah
Zidane angalie wapi alipokosea harafu aongeze juhudi
Sadick
Kwa sasa Real Madrid haina wachezaji wenye kiwango kusaidia timu kubaki kwenye ubora wake
Issa
Zidane kama timu imemshinda vile
Sabrina
Itapendeza sana ikirudi kwenye ubora wake
Latifa juma mohamed
Zidane inabid aongoze bidii
Sauda
Kila la kheri kwake
Carolyn
Zidane yupo vizuri
Angelina
Zidane namkubali sana
Rahma
Zidane namuelewa
aisha
Zidane kama madrid imemshinda atafute mbinu mbadala zaid
Saupha mohamed
Zidane yupo vizuri