Taarifa rasmi kutoka kwenye ukurasa wa Instagram wa TFF unaeleza kuwa dirisha la usajili na uhamisho wa kimataifa umefunguliwa rasmi leo.
Taarifa hiyo kutoka TFF inakuja ikiwa ni siku moja tu toka ligi kuu Tanzania bara maarufu kama VPL kumalizika jana na Simba kubeba kombe kwa mara ya nne mfulululizo.
TFF wameeleza kuwa dirisha hilo la usajili litakuwa wazi kwa ligi kuu VPL, Daraja la kwanza (FDL), Daraja la pili (SDL) na ligi ya wanawake ya Serengeti lite (SWPL).
Aidha TFF wameongeza kuwa dirisha hili la Usajili litafungwa rasmi Agosti 31 mwaka 2021 na hakutokuwa na muda wa ziada endapo timu zitakuwa hazijafanya sajili ndani ya muda huo.
Kasino ya Mayan Eagle inakukufanya kuwa bingwa wakati wowote unapoamua kuicheza. Utaburudika huku ukiendelea kutengeza mkwanja mrefu, jiunge sasa na uwe miongoni mwa mabingwa!!


