Borussia Dortmund wamekwea kileleni mwa ligi kuu ya ujerumani maaruga kama Bundesliga jana baada ya kuifunga klabu ya Hoffenheim bao moja kwa bila.
Katika mchezo uliopigwa katika dimba la Signal iduna park huo ulikua na kasi kwelikweli huku kila timu ikihitaji kupata matokeo ya alama tatu lakini Dortmund ndio walioweza kupata alama zote tatu baada ya goli la mapema la nahodha wa timu hiyo Marco Reus lililodumu mpaka mhezo kumalizika na kuwaeka kileleni mwa ligi hiyo.
Klabu hiyo inakaa kileleni kwa tofauti ya alama mbili baada ya kucheza michezo mitano na kuvuna alama 12 na kupoteza mchezo mmoja nafasi ya pili ni klabu ya Fc Bayern Munchen wenye alama kumi huku wakiwa na mchezo leo dhidi Union Berlin ambapo kama watapata alama tatu Dortmund watakwenda kuachia usukani wa ligi hiyo kwani Bayern watakua na alama 13 na kuongoza kwa tofauti ya alama moja.

