Baki wa Manchester City, Eric Garcia anaripotiwa kuwa anasubiri tu kujiunga na Barcelona kwa mkataba wa miaka mitano.

Mkataba wa sasa wa Garcia unaisha mwisho wa mwezi ujao, na Pep Guardiola alithibitisha awali kuwa nyota huyu hajakubali kusaini mkataba mpya, hivyo atakuwa anaelekea Barcelona.

Tangia hapo, staa huyu amekuwa akihusishwa na Barcelona, ambao walijaribu kumsajili katika hatua za mwisho za usajili wa mwezi Januari kabla ya dili hilo kuvunjika.

Hata hivyo, taarifa zinasema kuwa Barcelona tayari wameshafanya makubaliano ya awali na Garcia ya mkataba wa miaka mitano, hadi 2026. Hivyo nyota huyu wa miaka 20, anatarajia kurejea Catalonia.

Fununu zaidi zinasema kuwa Joan Laporta tayari ameshatoa ruksa ya staa huyo kuwasili Barcelona kama mchezaji huru, na anaweza kuwa mchezaji rasmi wa Barcelona mwisho wa msimu.

Garcia alitokea katika klabu ya ya Barcelona akijiboresha kufikia kikosi cha kwanza kabla ya kuondoka Man City mwaka 2017.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Garcia, Eric Garcia Kusaini Miaka 5 na Barcelona!, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa