Arsenal inaripotiwa wanalenga kukusanya £60m kwa mauzo ya wachezaji katika kipindi hiki cha majira ya joto kabla ya kampeni ya 2021-22 kuanza.

Baada ya kutolewa nje ya Ligi ya Uropa na Villarreal, pamoja na uwezekano finyu wa kumaliza katika nafasi saba za juu ya jedwali la Ligi Kuu, miaka 25 wa Gunners katika soka la Uropa inatarajiwa kufikia mwisho mwaka ujao.

Mikel Arteta inasemekana atasaidiwa na Stan Kroenke katika soko la uhamisho wa majira ya joto, na bosi wa Arsenal anafikiriwa kuwa anapanga marekebisho makubwa baada ya msimu huu mgumu kwao.

Kwa mujibu wa Football London, Washika bunduki watatafuta kuongeza kitita cha uhamisho wao kwa pauni milioni 60 msimu huu wa joto, na wachezaji wanaotajwa kuwkwa sokoni ni pamoja Bernd Leno, Hector Bellerin, Lucas Torreira, Sead Kolasinac, Ainsley Maitland-Niles na Matteo Guendouzi.

Pia kuna sintofahamu juu ya hatima ya Alexandre Lacazette na Eddie Nketiah, na Washika bunduki wanatajwa kumtazama fowadi wa Genk Paul Onuachu kama saini bora.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Arsenal, Arsenal Kukusanya £60m Kabla ya Msimu Mpya, Meridianbet

CHEZA HAPA

8 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa