Ratiba ya Manchester United wiki hii inaonesha watakutana na Leicester Jumanne kabla ya kumalizana na Liverpool siku ya Alhamisi na tayari wamejihakikishia kucheza Champions League msimu ujao.
Taarifa za vikosi:
Harry Maguire wa Manchester United ataikosa mechi ya ligi kwa mara ya kwanza tangu alipojiunga na United akitoke Leicester 2019 kutokana na tatizo la kifundo cha mguu.
Kocha Ole Gunnar Solskjaer atafanya mabadiliko zaidi pale atakapo kabiliana na Liverpool siku ya Alhamisi.
Leicester watakuwa bila Jonny Evans kufuatia kutolewa kwenye mchezo walipoteza kwa Newcastle siku ya Ijumaa kwa sababu ya tatizo la kisigino alilopata.
Harvey Barnes, James Justin na Wes Morgan bado wapo nje kwa sababu mbalimbali zikiwemo majeraha.
Rekodi za Kukutana:
Leicester wameshinda michezo miwili kati ya 29 katika Premier League dhidi ya Manchester United.
Mashetani Wekundu wamefunga katika mechi 23 zilizofuata za ligi kati ya pande zote tangu kipigo hicho, ambayo ni safu yao ndefu zaidi ya kufunga Ligi Kuu dhidi ya mpinzani mmoja.
Manchester United watakua na lengo la kushinda michezo ya nyumbani mitano mfululizo ya Premier League tangu mwaka 2018 mwezi March wakiwa chini ya Mourinho.
Marcus Rashford amefunga mabao matano ya Premier League dhidi ya Leicester idadi kubwa kuliko timu nyingine.
Leicester wameenda ugenini bila ushindi mfululizo michezo ya ligi kwa mara ya kwanza msimu huu.
Leicester wanaweza kuwa wa nne kuzifunga timu za Manchester ugenini kwa msimu mmoja baada ya Everton (1992-93), Middlesbrough (2003-04) na Liverpool (2008-09).
Kikosi cha Manchester United kinachoweza kuanza: Henderson; Tuanzebe, Lindelof, Bailly, Telles; Matic, McTominay, Van de Beek; Mata; Greenwood, Cavani
Kikosi cha Leicester City Kinachoweza Kuanza: Schmeichel; Amartey, Soyuncu, Fofana; Castagne, Ndidi, Tielemans, Thomas; Perez; Iheanacho, Vardy
Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.
Bonge la mechii
Man United win
Man u win
Man u win
Uchambuzi upo makini
Mechi mzur sana
Uchambuzi upo makini
Man u mkali
Man u wako makini San na ushindi juu
Man U win
Mechi ngumu kutabiri
Taarifa nzur