Kocha wa AC Milan, Stefano Pioli amewasilisha taarifa ya kutia moyo juu ya jeraha la hivi karibuni la Zlatan Ibrahimovic, huku mshambuliaji huyo wa Sweden anauguza jeraha kidogo kwenye goti lake.

Pioli Apokea Taarifa Nzuri Juu ya Majeraha ya Ibrahimovic

Mchezaji huyo wa miaka 39 alilazimishwa kuotoka baada ya dakika 66 katika ushindi wa 3-0 kwa Rossoneri dhidi ya Juventus.

Amepitia vipimo vya afya tangu wakati huo na, ameondolewa kwenye mechi mbili zijazo za Milan, Pioli amedokeza kwamba anaweza kurudi kabla ya msimu wa 2020-21 kukamilika.

Alipoulizwa juu ya maendeleo ya Ibrahimovic katika mkutano na waandishi kuelekea mchezo na Torino siku ya Jumatano,Pioli alisema: “Habari mbaya ni jeraha lake la goti.

“Hatopatikana kesho na Jumapili dhidi ya Cagliari, acha tuone maendeleo yake yatakuaje wiki ijayo.

Kumuona akiumia dhidi ya Juve kuliwafanya wengine waone kwamba msimu wake unaweza kuwa umekwisha na anaweza kukosa Mashindano ya Ulaya msimu huu wa joto.

Atakuwa na hamu kubwa ya kuongeza idadi ya michezo katika timu ya taifa 118 na, akiwa tayari ameongeza mkataba mpya na Milan kwa msimu ujao.


PESA IPO HAPA KATIKA KASINO YA LUCKY LUCKY.

Hii ndiyo burudani yenye ushindi! Ingia kwenye kasino ya Meridianbet kufukuzia ushindi huu. Cheza sasa Lucky Lucky na uwe moja ya washindi na Mabingwa.

Pioli, Pioli Apokea Taarifa Nzuri Juu ya Majeraha ya Ibrahimovic, Meridianbet

CHEZA HAPA

10 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa