Klabu ya Everton inayoshiriki ligi kuu ya Uingereza imefanikiwa kua timu iliyoruhusu magoli machache zaidi kwenye ligi hiyo mpaka sasa baada ya mizunguko minane.

evertonKlabu hiyo iliyo chini ya mwalimu Frank Lampard gwiji wa zamani wa klabu ya Chelsea ambaye aliichukua timu hiyo katikati mwa msimu uliomalizika na kufanikiwa kuinusuru timu hiyo isishuke daraja baada ya kua na matokeo mabovu.

Everton tangu kuanza ndo msimu imekua timu ambayo imeruhusu magoli machache zaidi baada ya kucheza michezo 8 na kuruhusu magoli 7 saba huku wakifuatiwa na vinara wa ligi hiyo klabu ya Arsenal,Brighton Hove and Albion, pamoja na klabu ya Newcastle ambao wote wameruhusu magoli nane.

Kutokana na hali hii inaonesha moja kwa moja sajili alizozifanya kocha Frank Lampard ndani ya Everton majira ya joto haswa kwenye ukuta wake imemlipa kwa kiwango kikubwa.

evertonTimu hiyo imemuongeza beki Conor Coady kutoka klabu ya Wolves pamoja Idris Gana Gueye kiungo wa ulinzi kutoka timu ya PSG sajili ambazo zimeleta mabadiliko makubwa kwenye timu hiyo ambayo ilionekana kuchechemea zaidi msimu ulimalizika lakini mpaka sasa wapo nafasi ya 11 baada ya kucheza michezo nane na alama zao 10.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa