Mlinzi wa klabu ya Leicester City Wesley Fofana anatarajia kutokuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo kitakacho menyana na klabu ya Chelsea siku ya Jumamosi kwenye mchezo wa ligi kuu ya nchini Uingereza.

Awali klabu ya Chelsea iliwasilisha offer tatu kwa mchezaji huyo ‘Wesley Fofana’ lakini zote zilikataliwa huku offer ya mwisho ikiwa na thamani ya kiasi cha £70million iliyowasilishwa siku ya Jumanne huku dirisha la usajili likitarajiwa kufungwa wiki ijayo.

Fofana, Fofana Nje Dhidi ya Chelsea, Meridianbet

Fofana kwa sasa anafanya mazoezi na timu ya vijana chini ya miaka 23, baada ya kukosekana kwenye mazoezi na timu ya wakubwa wiki iliyopita na hatajumuishwa kwenye kikosi cha Leicester City kitakachosafiri kwenda London kukipiga dhidi ya Chelsea siku ya Jumamosi kwenye uwanja wa Stamford Bridge.

“Mara zote imekuwa ni kujitoa, na wachezaji wakiwa tayari kujitolea kwa timu na maadili ya timu,” alisema Rodgers. “Imekuwa changamoto kwa Wesley, kama hauko kwenye mawazo sahihi, na unapaswa kuheshimu haki ya mchezaji, inapaswa kuendelea.

“Dirisha litafungwa muda sio mrefu na kila kitu kinabidi kiwe kimekamilika baada ya dirisha kufungwa. Hatakuwepo kwenye mchezo wa wikiendi. Anafanya mazoezi na timu ya vijana chini ya miaka 23.

“Sina uhakika , ikiwa kutakuwa na offer nyingine, akili yangu ni kwa wachezaji tulionao na timu. Siwezi kupoteza nguvu kufikiria sana kuhusu hilo. Ni jambo ambalo litafanywa na klabu. Mpaka hapo litakapotokea tunapaswa kufanya kazi na tulivyonavyo.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa