Doha: Timu ya taifa ya Argentina imeingia kwenye kumbukumbu ya kuuza zaidi tiketi kwenye michuano ya kombe la dunia inayotarajiwa kufanyika mwaka huu nchini Qatar kulingana na taarifa iliyotolewa na waandazi wa michuano hiyo.

Argentina kwenye mzunguko wa kwanza wanatarajia kukutana na Mexico November 26 na Saudi Arabia November 22, huku mchezo wao dhidi ya saudi Arabia ukiwa umeuza tiketi nyingi zaidi.

Argentina, Argentina Yaongoza Mauzo ya Tiketi Kombe la Dunia 2022, Meridianbet

Michezo yote itachezwa mbele ya mashibiki 80,000 kwenye uwanja wa Lusail ambao unatarajiwa kuchezewa mchezo wa fainali ya mwaka huu December 18.

FIFA mwezi huu walitoa takwimu ya idadi za tiketi zilizouzwa na kutaja kuwa mpaka sasa zaidi ya tiketi  2.45 million zilikuwa tayari zimeshauzwa kwa ajiri ya michezo ya awali.

Argentina na Mexico zimetajwa kama miongoni mwa nchi zilizonunua tiketi nyingi wakiwemo na Qatar, Marekani, Uingereza, Saudi Arabia, the United Arab Emirates, Ufaransa, Brazil na Germany.

Saudi Arabia vs Argentina ni mchezo wa pili uliouza tiketi nyingi kwenye michezo ya awali ya kombe la dunia 2022.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa