Mkurugenzi wa klabu ya Bayern Munich amethibitisha kua klabu hiyo itaingia sokoni katika dirisha dogo la usajili mwezi Januari ambapo wataboresha maeneo kadhaa katika kikosi chao.
Mkurugenzi Freund amesema timu hiyo inahitaji maboresho katika maeneo kadhaa hivo mwezi Januari lazima waingie sokoni kwajili ya kuboresha kikosi chao na kupambania mataji msimu huu.Bayern Munich ina mpango wa kuingia sokoni mwezi Januari na vipaumbele vya ni kiungo wa Ulinzi na beki wa katikati, Hii ni kutokana na taarifa ya mkurugenzi wa klabu hiyo bwana Freund ambaye ni mtendaji mpya klabuni hapo.
Klabu hiyo ambayo ipo chini ya kocha Thomas Tuchel toka mwezi Machi mwaka huu imekua haina mwenendo mzuri sana, Huku kiungo Joshua Kimmich akiwa hana mbadala wa uhakika klabuni hapo ndio sababu ya kuhitaji kumtafutia mtu wa kusaidiana nae majukumu.Aidha klabu ya Bayern Munich itaangazia beki wa katikati kwani klabu hiyo imekua ikruhusu mabao sana siku za karibuni, Hivo pia watahitaji kusajili beki mwingine wa katikati kwajili ya kuhakikisha wanatengeneza ukuta mgumu klabuni hapo.