Nyota wa klabu ya Arsenal na timu ya taifa ya Uingereza Bukayo Saka ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa kwenye michezo ya kirafiki kati ya Ivory Coast na Switzerland baada ya kukutwa na maambukizi ya Uviko-19.
Bukayo Saka siku ya jumanne alifanya mazoezi na kikosi cha timu kwa pamoja lakini hakuwa kwenye hali nzuri ya kuendela na mazoezi kwenye viunga vya St George Park.
Southgate hawezi kuongeza mchezaji wa kuweza kuziba nafasi ya saka kwenye hatua hii.
“Bukayo Saka ameondolewa kwenye kikosi cha timu ya taifa baada ya kupata maambukizi ya Uviko-19,” waraka wa FA ulisema.
“Mchezaji wa Arsenal amejitenga na kikosi kizima kilichopo St George Park tangu jumatano na sasa amerudishwa nyumbani. Na hakuna mchezaji wa kuziba pengo lake aliyepangwa kwenye kikosi cha wachezaji 24 kwa michezo ijayo.”
Mpaka sasa Southgate amepoteza wachezaji zaidi ya sita ambao ni Reece James, Trent Alexander-Arnold, Aaron Ramsdale, Tammy Abraham na Sam Johnstone kwa matatizo ya majeruhi.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.