Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa na klabu ya Paris Saint Germain Kylian Mbappe ametajwa kuwaa mchezaji mwenye thamani kubwa kuliko mchezaji yoyote kwa sasa baada ya kusajiri mkataba mpya na klabu hiyo hivi karibuni.
Mbappe ambaye kwa sasa anathamani ya £175.7million ambapo inamuweka juu ya mshambuliaji aliyesajiriwa hivi karibuni na klabu ya Manchester City Erling Haaland na mchezaji wa klabu ya Real Madrid Vinicius Junior.
Mbappe ambaye kwa sasa anaingiza kiasi cha £650,000 kwa wiki, mshindi huyo wa kombe la Dunia amekuwa akicheza kwenye ligi ya Ligue 1 tangu alivyoanza kucheza soka la kuklipwa. Huku CIES Football Observatory ikitoa Orodha ya wachezaji 20 wenye thamani kubwa ambapo Kylian Mbappe amekuwa kiongozi wa Orodha hiyo.
ORODHA YA WACHEZAJI 20 WENYE THAMANI KUBWA DUNIANI
1. Kylian Mbappe (£175.7m) – Paris St-Germain
2. Vinicius Junior (£158.4m) – Real Madrid
3. Erling Haaland (£130.4m) – Borussia Dortmund
4. Pedri (£115.5m) – Barcelona
5. Jude Bellingham (£114.3m) – Borussia Dortmund
6. Phil Foden (£106m) – Manchester City
7. Frenkie de Jong (£96.2m) – Barcelona
8. Luis Diaz (£94m) – Liverpool
9. Ruben Dias (£93.7m) – Manchester City
10. Ferran Torres (£93.6m) – Barcelona
11. Lautaro Martinez (£91.2m) – Inter Milan
12. Jamal Musiala (£90m) – Bayern Munich
13. Jadon Sancho (£88.2m) – Manchester United
14. Mason Mount (£85.7m) – Chelsea
15. Bukayo Saka (£85.7m) – Arsenal
16. Josko Gvardiol (£85.3m) – RB Leipzig
17. Bruno Fernandes (£83.6m) – Manchester United
18. Nicolo Barella (£81.1m) – Inter Milan
19. Kai Havertz (£80m) – Chelsea
20. Joao Felix (£77.6m) – Atletico Madrid
SHINDA Samsung A32 ukiwa na mchezo wa Aviator kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet! Kwea pipa ukusanye zawadi zako pamoja na ushindi mnono wa mkwanja!