Ac Milan Kumuhitaji Abraham

Klabu ya Ac Milan inaelezwa ipo kwenye mipango ya kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Chelsea Tammy Abraham ambaye kwasasa anakipiga ndani ya klabu ya As Roma.

Ac Milan inahitaji mshambuliaji mwingine ndani ya kikosi chao kuelekea msimu ujao na Tammy Abraham anaonekana kua chaguo namba moja kwa klabu hiyo, Hivo miamba hiyo ya soka nchini Italia ili ifanikiwe kupata saini ya mshambuliaji huyo ni kulipa ada sahihi ambayo itahitajika na klabu ya As Roma.ac milanMshambuliaji Tammy Abraham inaelezwa yuko tayari kujiunga na Rosonneri kuelekea msimu ujao na kinachosubiriwa ni majadiliano ya vilabu viwili, Ambapo makubaliano ya timu hizo yakifikiwa ni wazi mshambuliaji huyo anakua na nafasi kubwa ya kujiunga na Ac Milan.

Tammy Abraham ambaye ameitumikia klabu ya soka ya As Roma kwa takribani misimu mitatu sasa na akicheza kwa kiwango kikubwa ndani ya timu hiyo, Kitu kikubwa kilichofanya klabu ya Ac Milan kumuona kama mtu sahihi ndani ya timu hiyo kuelekea msimu ujao.

Acha ujumbe